Ukumbi Wa Mashirikiano Duniani – Nairobi
Kwa Jina La
Mungu
Kuwakumbuka walioadhiriwa na siasa kali za Kidini
Tahadhari!
Msalaba Utavumbuliwa!
+ Msalaba huu unapinga ugandamizaji
dhidi ya utumiaji wa vibonge vya kuzuhia uzazi na elimu ya uzalishaji.
+ Msalaba huu haubagui dhidi ya utuoji
mamba au sayansi ya utafiti wa uzazi bila ngonobali unaotetea haki za wanawake
wote duniani
+ Msalaba huu umeundwa na Msanii Jens
Galschiot kutoka Denmark.
Twahijitaji wasaidizi na watu ambao tuweza kufanya nao duniani, wasililiana
kwa njia ya barua pepe – aidoh@aidoh.dk ama
anagalia www.aidoh.dk/InTheNameOfGod
Sanamu Hii
ya Msalaba
Huu msalaba unatokana na sanaa ya uchongaji na ni sanamu tu. Sanamu hii
imechongwa kwa kutumia nishani ya shaba nyekundu na imebandikwa jina ‘In
the Name of God” (“Kwa Jina La
Mungu”). Huu msalaba ni chombo kinachowakilisha haki za kutumia vibonge vya
kupanga uzazi na kutokuwa na ubaguzi dhidi ya elimu ya uzazi.
Historia
Tangu jadi, msalaba kama sanamu umetumiwa vibaya na wanaoipinga bibilia kwa
kusema kuwa bibilia inakubali ngono bila ukingaji. Katika hii sanaa, sanamu hii
inaonyesha kijana wa makamo ambaye si mweupe au mweusi na ambaye ni mjamzito.
Kijana huyu ametundikwa msalabani akisulubiwa. Hadhma yake kuu ni kuchangia
katika mjadala kuhusu vidonge vya kuzuhia uzazi (contraceptives) au uabaguzi dhidi ya elimu ya kizazi iliyochangiwa
na sayansi (stem cell research) na si
siasa kali za kidini (religious
fundamentalism).
Kwa mara ya kwanza sanamu hii ilionyeshwa katika Kanisa Kuu lililoko katika
mjii mkuu wa Denmark, Copenhagen mnamo tarehe 01.12.2006. Mkuu wa kanisa hilo
Bw. Anders Gadegaard alinukuliwa akisema:
“Tunaungana
na wasanii walioichonga sanamu hii hili kuthibitisha kuwa sisi hatuungani kamwe
na wanaokataa bibilia kuchangia katika mjadala wa utumiaji wa vibonge vya uzazi
katika mjadala wa upangaji uzazi na elimu ya uzalishaji”
(Tafsiri)
Msalaba huu utavumbuliwa sehemu mbali mbali hapa Nairobi wakati wa mkutano
wa kimataifa wa kushirikiana (World
Social Forum). Baadaye utafumbuliwa huko Vatican, Marekani na nchi zingine
ulimwenguni.
Huu ni msalaba unaotetea haki za kutumia vibonge vya kupanga uzazi.
Rais wa Marekani Bw. George w. Bush na wakuu wa Kanisa la Kikatoliki
wameungana kusurutisha ulimwengu mzima kuaamini kuwa kinga ya pekee dhidi ya
uneeezaji wa maradhi ya ukimwi na mimba ovyo ni kutoshiriki katika ngono.
Tayari, msimamo huu wao usio na msingi wa kisayansi umechangia kubuniwa sera
mbaya barani Afrika, Asia na Marekani ya Kati ambako mamilioni ya watu
wameadhiriwa na ukimwi, maradhi ya zinaa na utoaji wa mamba. Maoni zaidi kutoka
Vatican yanaweza kupatikana katika mtandao www.vatican.va
.
Msanii Jens Galschiot
Jens Galsciot alizaliwa 1994 huko Odense Denmark. Anajulikana sana kutokan
na kazi zake za kipekee zinazoegemea tofauti za kiuchumi kote ulimwenguni. Kazi
zake za sanaa zimewahikuonyeshwa katika
bara la ulaya (European Cities ’93), Hong Kong, Mexico na Brazil.
Miradi yake inafadhiliwa mauzo ya sanaa yake na michango kutoka kwa
wafadhili wa kibanfsi, mashirika yasiyo ya serikali na vyama vya wafanyi kazi.
Bw. Galschiot amenukuliwa akisema:
“Sanamu
hii haipingani na dini ya kikristo ulimwenguni. Nakubiliana na wote
wanoyachukua maadili meme ya bibilia. Hata hivyo, sanamu hii kamwe haikubaliani
na wanoegemea siasa au tafsiri kali ya bibilia ambayo ndio imeendelea
kuchangaia masaibu mengi dhidi ya watu wengi duniani.
Pia
sanamu hii haisemi utuoaji wa mamba uhalalishwe. Inatetea haki zinazoambatana
elimu bora ya uzazi” (Tafsiri)
Mkutano (World Social Forum)
Kutakuweko na sanamu mbili katika mkutano wa Nairobi unaoanza tarehe
20.01.2007. Pamoja na wasanii kutoka Kenya Uganda, kutakuwa na asana ya
uigizaji na mijadala kuhusu swala hili.
Mchango na Ushirikiano
Mradi huu unahitaji msaada na/au mchango wa wafadhili, washirika na wasanii
kote ulimwenguni. Msaada huu utawezesha msalaba huu kuzulu nchi zingine
ulimwenguni hili kuboresha mjadala wenyewe.
Tunatarajia kuwa mashirika ya wanawake, vijana, sanaa, au yale yanayohusika
na sera ya upanganji uzazi, uteteaji wa haki za kibinadamu, vyama vya kisiasa
na watu binafsi watependezwa, kuuchangia na kuusaidia mradi huu.
Mradi huu umebuniwa na wasanii wanaojitegemea na ambao hawana mlengo wowote
wa kisiasa au kidini. Kazi yetu inahitaji wahisani, washiriki na wasanii kamaa
wewe.
Unaweza kuufuatilia mjadala wa sanamu hii kwa kuuangalia mtandaowetu ambao
ni www.aidoh.dk/InTheNameOfGod
au www.aidoh.dk/GlobalGag kwa
habari zaidi za kimataifa. Ama, jiunge nao kwa kutaandikia barua pepe katika aidoh@aidoh.dk
www.aidoh.dk/wsf2007
Wakati wa mkutano wa Nairobi
Msanii Jens Galschiot anaweza kupigiwa simu katika nambari 0728 947 393 au 0728
947 390 au kwa barua pepe aidoh@aidoh.dk
Jens Galschiot – sculpteur,
Banevaenget 22 – DK-5270 Odense N – Danemark
Tél.+45 6618 4058 –
Fax +45 6618 4158
Email: aidoh@aidoh.dk
– Internet: www.aidoh.dk